Tuesday, May 5, 2020



SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF), limetoa angalizo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu mgawo wa dola laki tano (zaidi ya Sh bilioni moja) zinazotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa nchi wanachama ili kunusuru anguko la uchumi kutokana na janga la Corona.

Akizungumzia ishu hiyo, msemaji wa shirikisho hilo, Adam Natepe, ameitaka TFF kuwagawia sehemu ya fedha hizo kama katiba za TFF na ZFF zinavyoelekeza.


 “TFF inapaswa kutupatia sehemu ya mgawo wa Fifa kama katiba zetu zinavyoelekeza, kwa sababu tunawatazama wao kwenye upande wa uwakilishi wa kimataifa, hivyo basi hilo liko wazi na wanapaswa kutupatia sehemu ya fedha hizo zinazotolewa na Fifa ili kunusuru uchumi wa ZFF katika kipindi hiki cha Corona,” alisema Natepe.

ZFF na TFF zimekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu kuhusu masuala ya kifedha kuanzia kwenye mgawo wa Fifa, Caf na hata ada za usajili wa wachezaji wanaosajiliwa kutoka visiwani Zanzibar, kwenda kwenye timu za Ligi Kuu Bara.

0 comments:

Post a Comment