LIVERPOOL iliyo chini ya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp inapewa nafasi kubwa ya kusepa na Kombe la Ligi Kuu England msimu huu wa 2019/20.
Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 82 baada ya kucheza mechi 29 mabingwa watetezi Manchestyer City wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 28.
Kinara wao wa utupiaji ni Mohamed Salah raia wa Misri huku timu ikiwa imetupia mabao 66.
Ametupia jumla ya mabao 16 na Ligi inatarajiwa kurejea Juni bila mashabiki na kuna taarifa kwamba zitapunguzwa dakika 90 ili ziwape muda wachezaji wa kupumzika kutokana na kulazimika kucheza mechi tatu ndani ya wiki ili kumaliza msimu ambao ulisimamishwa kwa muda kutokana na janga la Virusi vya Corona.
0 comments:
Post a Comment