UONGOZI wa Arusha FC, inayoshiriki Ligi Dajaja la Kwanza umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzitazama timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza pamoja na zile za madaraja ya chini ili kuwapa sapoti ya kuweza kumalizia mechi zilizobaki kutokana na kuyumba kiuchumi.
Akizungumza na BLOG HII, Ofisa Habari wa AFC, Bahati Msilu amesema kuwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza hazina wadhamini ni mali ya mashabiki jambo linalowafanya wawe kwenye wakati mgumu kumaliza mechi zao iwapo ligi itarejea.
"Tulikuwa tumepanga bajeti ya kumaliza ligi ambapo mechi zetu nne bajeti yetu ilikuwa milioni 14 kibindoni baada ya shughuli kusimama mambo mengi kwetu pia yalisimama hakuna fedha.
"Kikubwa ambacho ninakiomba kutoka kwa TFF waangalie namna ya kuweza kutupa sapoti iwe kwa fedha kwa ajili ya kumalizia mechi hizi maana tumefurahia tamko la Rais John Magufuli kufikiria kwamba ligi inaweza kurudi hivi karibuni," amesema.
Ligi zote zilisisimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Recent Posts
- LIVERPOOL INA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA ENGLAND, KUNA MPANGO WA KUPUNGUZA DAKIKA 90 LIVERPOOL iliyo chini ya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp inapewa nafasi kubwa ya kusepa na Kom...Read more
- ZFF WATOA ANGALIZO TFF MGAWO WA MAMILIONI YA FIFA SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF), limetoa angalizo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)...Read more
- TFF YAZIKUMBUSHA KLABU NCHINI KUTOANZA MAZOEZI HADI SERIKALI ITAKAPOTOA TAMKO RASMI ...Read more
- Tetesi za soka leo Mei 5 Liverpool wamewaambia wawakilishi wa Timo Warner,24, kuwa wanahitaji muda zaidi ili kuamua kama...Read more
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.