Mabingwa wa soka DR Congo TP Mazembe wamekataa ofa ya dola milioni 2 za kimarekani kutoka kwa mabingwa wa kihistoria barani Afrika Al Ahly, kwa ajili ya usajili wa nyota wao Jackson Muleka.
Uongozi wa TP Mazembe umekataa ofa hiyo, na bado haujasema lolote kama utaendelea kusubiri ofa mpya kutoka kwa Al Ahly, ambao wameonyesha dhamira ya kukiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
Muleka ameshaifungia TP Mazembe jumla ya mabao 60 katika misimu miwili iliyopita, katika mashindano yote.
Jana mabingwa hao wa kihistoria barani Afrika (Al Ahly), waliripotiwa kuwa katika harakati za kumuwani mshambuliaji kutoka nchini Uruguay na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Leandro Gastón Sirino Rodríguez.
Gastón mwenye umri wa miaka 29 amehusishwa na mipango ya kuwa mbioni kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria Afrika, kufuatia kuwa kwenye kiwango bora tangu alipotua Mamelodi Sundowns akitokea FC Bolivar ya Bolivia Januari 2018.
Mshambuliaji huyo amecheza vyema kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kuwa mchezaji aliye na nafasi kubwa wakati wa msimu wa 2019/20 kwa Masandawana, na Al Ahly tayari imetupa nyavu zake kumpeleka jijini Cairo kabla ya msimu ujao.
Imeripotiwa kuwa ofa ya kwanza ya Ahly ni Pesa na kumtoa Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Angola, Geraldo ambaye ameshindwa kufikia kiwango kilichotarajiwa na magwiji hao wa Cairo-Misri.
Tayari Geraldo ameshacheza michezo 10 bila kuhusika na goli lolote, na kama mambo yatakwenda kama yanavyotarajiwa atashuka bondeni (Afrika Kusini) ili kukamilisha uhamisho wa Gaston Sirino ambaye ameshaituikia Mamelodi Sundowns katika michezi 90 na kufungwa mabao 22 na kutoa pasi za mwisho 26
0 comments:
Post a Comment