Friday, September 11, 2020


Gareth Bale ataendelea kusalia Real Madrid mara baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili rabda klabu hiyo ya Hispania ilipe mkataba wake.

Nyota huyo anaonekana kama vile amekwama ndani ya Real Madrid huku ikidaiwa kuwa klabu hiyo imeridhia kumpa nusu mshahara kama endapo ataondoka kwa mkopo.

Hata hivyo hakukuwa na mawasiliano yoyote baina ya mchezaji huyo na klabu yake huwenda ombi hilo litamfanya Bale kuendelea.

Bale anaingiza paundi milioni 15.2 kwa msimu na amesalia na miaka miwili, hii inamaanisha Madrid watapaswa kutafuta paundi milioni 60 ili kumpatia Bale kama wataachana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales.

 

0 comments:

Post a Comment