Friday, October 2, 2020

 



UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya wao leo kuifuata JKT Tanzania, Dodoma kwa basi ni kutimza ombi la mashabiki wao wa Morogoro ambao waliwaomba wawapelekee taji la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa msimu wa 2019/20.


Simba leo inaanza safari kuifuata JKT Tanzania, Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatimiza maombi ya mashabiki wao wa Morogoro ambao wameomba wapelekewe taji la ligi.


"Kikosi kitaondoka kwa basi kuelekea Dodoma na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutimiza ombi la mashabiki wa Morogoro ambao waliomba tuwapelekee taji letu la ligi ambalo tulitwaa msimu uliopita.

"Hivyo kwa kukubali ombi letu la mashabiki wa Morogoro tutakuwa na kombe letu, mashabiki watapata muda wa kuliona kombe letu na Jumamosi tutaanza safari kuelekea Dodoma ambapo tutapata muda wakufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuikabili JKT Tanzania," amesema.

0 comments:

Post a Comment