Saa 3 zilizopita
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Diego Maradona - akionesha kombe la dunia 1986, wakati wa mazoezi pamoja akiwa na mkewe wa zamnai Claudia na mwanawe wa kike Dalma na Gianina
Umaarufu wake pekee haumtendei haki,. Diego Maradona alikuwa mchezaji mwerevu kupita kiasi katika uwanja wa mpira na mtu aliyezua utata.
Kutoka nchini anakotoka Argentina hadi ufanisi alioupata Itali, ushindi wake wa kombe la dunia na utumizi wa mihadarati uliomuangusha , tazama maisha yake katika picha.
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Maradona alicheza mechi ya fainali ya kombe la dunia akiiwakilisha Argentina mwaka 1982 nchini Uhispania lakini alikuwa maarufu miaka minne baadaye.
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Kulikuwa na utulivu kabla ya kimbunga: Walisaliamiana kwa mkono na kipa wa England Peter Shilton kabla ya kombe la mechi ya robo fainali ya kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Goli la hand of Gold dhidi ya England , lilifuatiwa na goli bora la Karne.
CHANZO CHA PICHA, REX FEATURES
Maelezo ya picha, Alikuwa mchezaji wa kivyake: Maradona alitangazwa kuwa mchezaji bora wa FDimba hilo la Dunia baada ya kuisaidia Argentina kupata ushindi 1986, mbali na kuisaidia timu hiyo kufika fainali miaka minne baadaye.
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Alikuwa mfalme: Maradona alikuwa mchezaji nyota na maarufu katika klabu ya Naoli nchini Itali ambapo alijishindia Kombe la Uefa mwaka 1989 pamoja na mataji mawili ya ligi. Tishati Nambari 10 ilihifadhiwa kwa niaba yake
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Maradona, katika picha hii ya 2001, alitatizika na utumizi wa dawa za kulevya na masuala ya kuongeza uzito
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Maradona, akiwa kocha wa taifa wa Argentina akitoa hekima yake kwa mshambuliaji Lionel Messi katika kombe la Dunia la 2010 ambapo walishindwa kwa magoli 4-0 na Ujerumani katika awamu ya robo fainali
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Maradona akipiga picha na bango la picha yake wakati ambapo timu yake ya taifa Argentina ilikuwa ikicheza dhidi ya Nigeria katika kombe la Dunia lililoandaliwa Urusi 2018.
0 comments:
Post a Comment