KOCHA SIMBA APATA TIMU YA KUFUNDISHA AFRIKA KUSINI
DYLAN Kerr aliyewahi kuinoa Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara amepewa kibarua cha kuinoa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Kerr mwenye miaka 53 ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa aliwahi kuinoa Klabu ya Baroka FC msimu wa 2020 ambapo aliibuka ndani ya klabu hiyo akitokea Klabu ya Black Leopards.
Pia aliwahi kuifundisha Klabu ya Gor Mahia msimu wa 2017/18 nchini Kenya baada ya kuchimbishwa ndani ya Simba aliyoifundisha msimu wa 2015/16.
Black Leopards imemrejesha tena Kerr ndani ya kikosi hicho baada ya kumfuta kazi Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye naye aliifundisha Simba kwa msimu wa 2019/20 na aliweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Akiwa ndani ya timu hiyo alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi tatu na zote alipoteza jambo ambalo limewafanya mabosi wa timu hiyo kumfuta kazi jumlajumla.
Habari kutoka Afrika Kusini zimeeleza :"Kerr atafanya kazi na Morgan Shivambu na Mongezi Bobe akichukua mikoba ya Aussems," ilieleza taarifa hiyo.
Ndani ya Baroka FC, kocha huyo alifutwa kazi hivyo anarejea kwenye timu yake ya zamani akiwa huru
0 comments:
Post a Comment