DUNIA inamtambua mzee wa kuvunja rekodi Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika za lala salama wakati Manchester United ikiitungua mabao 2-1 Villarreal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbele ya mashabiki 73,130 waliohudhuria Uwanja wa Old Trafford Ronaldo alivunja rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa amefanya hivyo mara 178 na bao lake la dakika ya 90+5 likiipa pointi United katika kundi F.
Ni Paco Alcacer alianza kufunga dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti ila lilisawazishwa na Alex Telles kisha bao la ushindi likawekwa kimiani na mnyama Ronaldo ambaye aliivunja rekodi ya Iker Casillas aliyekuwa anashikilia rekodi ya kuwa nyota ambaye amecheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kucheza mechi 177 huku mshikaji wake Lionel Messi ambaye yupo PSG amecheza mechi 151 akiwa ni namba tatu.
Mvunja rekodi huyo ameifanya United kukusanya pointi tatu kwa mara ya kwanza ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa nafasi ya tatu huku vinara wakiwa ni Atalanta wenye pointi nne. Katika mchezo huo ni David de Gea kipa wa Manchester United aliibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment