Mcheza Tennis, Casper Ruud wa Norway amefanikiwa kuibuka na Ubingwa wa mashindano ya San Diego Open nchini Marekani alfajiri ya kuamkia leo Oktoba 4, 2021 baada ya kumfunga Muingereza Cameroon Norrie 6-0 kwa 6-3.
Baada ya kubeba ubingwa huo, Ruud amesema; "Kwa kawaida, Daniil (Medvedev) na Novak (Djokovic) wana mataji makubwa, Kwahiyo ningependa kufanikiwa zaidi yahapa hata kushinda Grand Slam tatu zaidi”
“Litakuwa ni jambo jemakumaliza mwakana makombe mengi, siwezi kudanganya kuhus hilo”. Alisema Ruud.
Ruud anayeshika nafasi ya pili kwa Ubora nchini Norway ameonesha kiwango safi na kubeba ubingwa huo unaomfanya awe mchezaji pekee mwenye makombe mengi ndani ya msimu mmoja, makombe 5 na kumpiku Novak Djovokic.
Kwa upande wa Cameroon Norrie amekuwa na kampeni ya kinyonge baada ya kucheza fainali tano na kushinda ubingwa mmoja pekeeake.
0 comments:
Post a Comment