Luis Suarez amesisitiza kuwa aina yake ya ushangiliaji kama vile ‘kupiga simu’ wakati akiifungia Atletico Madrid kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Barcelona ulikuwa aumuhusu kocha Ronald Koeman.
Mshambuliaji huyo 34, hakusherehekea goli lake mbele ya waajiri wake wa zamani Barca lakini alionekana kama vile akituma meseji ya simu kwa Koeman kwa aina ya namna alivyoweka mkono wake wa kulia kanakambwa anapiga simu.
Ronald Koeman ambaye kwa sasa amekalia kuti kavu pale Barcelona aliwahi kumpia simu Suarez na kumwambia hayupo kwenye mipango yake wakati huo kabla hajajiunga na Atletico Madrid, hivyo ni kama vile Suarez amemkumbushia tukio hilo baada ya kuwafunga.
Baada ya mchezo huo, Suarez alisema kuwa alama hiyo inawawakilisha watoto wake watatu na wala hamchimbi bosi wake huyo wa zamani, Koeman.
0 comments:
Post a Comment