Sunday, October 17, 2021

 



BAO pekee la beki wa kimataifa wa England, Ben Chilwell dakika ya 45 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford Uwanja wa Brentford Community, Brentford, Middlesex.
Kwa ushindi huo kwenye mchezo ambao kipa Msenegal, mzaliwa wa Ufaransa, Edouard Mendy alijizolea sifa kemkem kwa kuokoa michomo mingi, Chelsea inafikisha pointi 19 na kurejea kileleni sasa ikiizidi pointi moja Liverpool baada ya wote kucheza mechi nane.

0 comments:

Post a Comment