WENYEJI, Watford FC wametandikwa mabao 5-0 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road, Watford.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na washambuliaji Msenegal, Sadio Mané dakika ya tisa, Mbrazil Roberto Firmino dakika ya 37, 52 na 90 na Mmisri Mohamed Salah dakika ya 54.
Liverpool wanafikisha pointi 18 baada ya ushindi huo kwenye mchezo wa nane na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Chelsea ambayo baadaye itamenyana na Brentford.
0 comments:
Post a Comment