Sunday, October 17, 2021

 



MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wameanza vyema michuano ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana.
Shujaa wa Simba SC leo ni Nahodha, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco aliyefunga mabao yote mawili dakika ya tatu na ya sita mara zote akimalizia mipira iliyookolewa baada ya kona.
Simba watahitaji kuulinda ushindi wao kwenye mechi ya marudiano Jumapili ijayo ili kwenda hatua ya makundi.

0 comments:

Post a Comment