Sunday, October 17, 2021



MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Adam Paul Salamba amejiunga na klabu ya JS Saoura ya Algeria kutoka Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.
Salamba ametambulishwa wiki hii na tayari ameanza kazi katika klabu hiyo hiyo mpya yenye kumbukumbu nzuri za huduma ya Mtanzania mwingine, Thomas Emmanuel Ulimwengu.
Salamba aliibukia Stand United mwaka 2016 kabla ya kwenda Lipuli FC mwaka 2017, Simba SC 2018, Al-Jahra SC ya Kuwait 2019 na Namungo FC 2020.

0 comments:

Post a Comment