GEORGINIO Wijnaldum nyota wa PSG ameweka wazi kuwa hana furaha ndani ya kikosi hicho kwa kuwa anapita katika nyakati ngumu.
Kiungo huyo amesajiliwa na PSG msimu huu akitokea Liverpool akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumeguka ndani ya Anfield.
Baada ya kutua PSG yenye Lionel Messi, Neymar Jr amecheza mechi 11 katika michuano yote bila kufunga wala kutoa pasi ya bao.
Kocha Mkuu wa PSG, Mauricio Pochettino amekuwa akiwatumia Marco Verrati na Idrissa Gueye katika nafasi ambayo anacheza kiungo huyo.
0 comments:
Post a Comment