Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemueleza kocha wa sasa wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer kwamba wakati wote anapaswa kuwatumia wachezaji wake bora
Ferguson amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu Ole amuweke benchi nyota wake Cristiano Ronaldo katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Everton mwishoni mwa wiki.
Ronaldo aliingia dakika 33 za mwisho hata hivyo alishindwa kuisaidia timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Everton iliyoonekana kuimarika katika mchezo huo. Anthony Martial aliitanguiliza United kwa bao a dakika ya 43 kabla ya Andros Townsend kuisawazishia Everton katika dakika ya 65.
Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, United ilishindwa kupata bao la ushindi ambapo wengi waliamini kwamba kama angemuanzisha Ronaldo katika mchezo huo uliosukumizwa katika dimba la Old Traford.
Katika mchezo huo pia Ole aliwaanizisha benchi kiungo mfaransa Paul Pogba na mshambuliaji wa poembeni wa England Jadon Sancho.
Kwenye video moja wakati akizungumza na bingwa wa UFC Khabib Nurmagomedov kwenye uwanja wa Old Trafford, Sir Ferguson alisikika akisema "siku zote anzisha wachezaji wako bora".
Video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram wa Nurmagomedov, unaonyesha Ferguson akisema Everton 'Toffees' walipata mteremko baada ya kuona Ronaldo hachezi..."
Baadae Nurmagomedov alimkumbusha Ferguson kwmaba Ronaldo aliingia katika kipindi cha pili, kabla ya Fergie kusema wachezaji wa haiba ya Ronaldo hawapaswi kukaa nje, wanapaswa kuanza kikosi cha kwanza.
Baada ya filimbi ya mwisho, Ronaldo alionekana kutoka uwanjani akiwa amechukia na kuzungumza mwenyewe.
"Ukiwa na Cristiano Ronaldo, unapaswa kutengeneza timu na mfumo kumzuguka yeye,ili acheze vyema," alisema mshambuliaji wa zamani wa England Arsenal Ian Wright.
Lakini Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alitetea uamuzi wake wa kumpumzisha nahodha huyo wa Ureno mwenye miaka 36.
"Mimi na yeye tunafahamu zaidi kuliko wachambuzi,"alisema Solskjaer."Inahusu ni wakati gani mzuri acheze ama asicheze, sio mtoto mdogo kwa sasa, ni mchezaji mkubwa wa kulipwa na yuko tayari kuingia na aliingia akiwa vizuri na nguvu."
Wakati huo huo, kocha msaidizi wa United Mike Phelan amesaini mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2024.
Phelan alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Ferguson kabla ya kurejea Old Trafford mara baada ya Solskjaer kuteuliwa kuwa kocha wa muda mwezi Disemba mwaka 2018.
United wanapambana kuwaongezea mikataba makocha wengine wa kikosi cha kwanza Michael Carrick na Kieran McKenna.
0 comments:
Post a Comment