TANZANIA imekamilisha mechi zake za Kundi B michuano ya COSAFA kwa wanawake kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Sudan Kusini Jumatatu Uwanja wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Jijini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Mabao yote ya Twiga Stars yote yamefungwa na beki Stumai Abdallah Athumani ambaye mwisho wa mchezo alipewa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi.
Mechi za awali, Twiga Stars ilishinda 3-0 dhidi ya Zimbabwe na 2-0 dhidi ya Botswana na kwa kumaliza kama kinara wa Kundi B itakutana na mshindi wa pili wa Kundi A kwenye Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment