Wednesday, October 13, 2021

 



WENYEJI, England wamelazimishwa sare ya 1-1 na Hungary katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
Hungary walitangulia kwa bao la penalti la Roland Sallai dakika ya 24 baada ya rafu iliyochezwa na Luke Shaw, kabla ya John Stones kuisawazishia Three Lions dakika ya 37.
Kwa sare hiyo, England inafikisha pointi 20 na kuendelea kuongoza Kundi I, ikifuatiwa na Poland yenye pointi 17, Albania 15, Hungary 11, Andorra sita, wakati San Marino inashika mkia ikiwa haina pointi baada ya mechi nane.

0 comments:

Post a Comment