Monday, October 25, 2021

 


HATMA ya Biashara United kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ipo mikononi mwa Bodi ya Kandanda Afrika (CAF) kufuatia jana kushindwa kutokea uwanjani Jijini Benghazi nchini Libya kumenyana na wenyeji, Al Ahly Tripoli katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili kwa matatizo ya usafiri.
Mwenyekiti wa Biashara United, Suleiman Mataso alisema jana kwamba ndege waliyoomba kusafiri nayo awali iliahirisha safari hiyvo wakalazimika kukodi ndege ya shirika la Tanzania (ATCL), lakini wakakosa vibali vya kutua kwenye nchi ambazo wangepitia kabla ya kutua Benghazi.
Baada ya hapo Biashara msaada Shirikisho la Soka Tanznaia (TFF) kuwaombea CAF mechi yao isogezwe mbele hadi Jumanne ili wapate vibali vya anga vya kutua kwenye nchi watakazopitia.


Hata hivyo jana taratibu zote za mchezo zilifuatwa Uwanja wa Martyrs of February Jijini Benghazi baada ya wenyeji Al Ahli kufika na baada ya muda wa kikanuni, waamuzi wakamaliza mchezo kwa tafsiri Biahsara haikutokea uwanjani.
Lakini jana usiku TFF ilitoa taarifa  kwamba bado wanasubiri majibu kutoka CAF kuhusu ombi la kusogezwa mbele mchezo huo.
Ikumbukwe mechi ya kwanza Biashara United inayofundishwa na kocha Mkenya, Patrick Odhiambo anayesaidiwa na mzawa, Marwa Chamberi ilishinda 2-0 mabao ya Deogratius Judika Mafie dakika ya 40 na Atupele Green Jackson dakika ya 61.


0 comments:

Post a Comment