Monday, October 25, 2021

 



WENYEJI, Manchester United wameadhibiwa vikali na mahasimu, Liverpool baada ya kuchapwa mabao 5-0 jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Mabao y Liverpool yamefungwa na Naby Keita dakika ya tano, Diogo Jota dakika ya 13 na Mohamed Salah matatu dakika ya 38, 45 na ushei na 50.
Manchester United ilimaliza pungufu baada ya Paul Pogba aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mason Greenwood kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Keita dakika ya 60.
Liverpool inafikisha pointi 21 na kusogea tena nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na Chelsea, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 14 katika nafasi ya seba baada ya timu zote kucheza mechi tisa.

0 comments:

Post a Comment