Monday, October 25, 2021

 

WENYEJI, Barcelona wamechapwa mabao 2-1 na mahasimu wao, Real Madrid katika mchezo wa La Liga jioni ya leo Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
Mabao ya Real Madrid yamefungwa na David Alaba dakika ya 32 akimalizia pasi ya Rodrygo na Lucas Vázquez dakika ya 90 na ushei dakika nne kabla ya 
Sergio Agüero kuifungia Barca la kufutia machozi katika muda wa ziada.
Real Madrid inafikisha pointi 20 na kupanda kileleni mwa La Liga ikizizidi wastani wa mabao tu Sevilla na Real Sociedad, wakati Barcelona inabaki na pointi zake 15 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi tisa.


0 comments:

Post a Comment