Monday, October 25, 2021

 

g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kipigo walichokipata Manchester United cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool katika ligi kuu ya England, imekuwa habari kubwa ya soka mwishoni mwa wiki hii, na kuzima hata taarifa za kunyanyaswa kingono kwa beki wa zamani wa timu hiyo Patrice Evra na ile ya Chelsea Jumamosi kuichapa Norwich 7-0.

Kipigo hicho kimezima pia taarifa za mechi ya El clasico, katika 'La liga' Real Madrid ikiifunga Barcelona nyumbani kwao Camp Nou kwa mabao 2-1, Kun Aguero akifungua kabati la mabao kwenye maisha yake mapaya Barca. Ikazima pia taarifa za mechi kabambe ya Seria A kule Italia Juventus ikienda sare ya 1-1 na AC Milan, Juventus ikisawazisha katika dakika za lala salama kupitia kwa Paulo Dyabala.

Lakini ukubwa zaidi wa kipigo cha Manchester umebebwa na kiwango cha Mohamed Salah, mshambuliaji wa Liverpool aliyehusika katika mabao manne kati ya matano, akifunga matatu na kutengeneza bao moja la Naby Keita katika dakika ya 5.

Ni hat-trick ya kwanza kufungwa Old Trafford na mchezaji wa timu pinzani katika ligi kuu tangu Januari 1, 1992 Dennis Bailey alipoifungia QPR dhidi ya Manchester United.

aaa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mo Salah akishangilia moja ya mabao yake aliyofunga dhidi ya Manchester United

Kwa mabao hayo Mohamed Salah amevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika katika historia ya ligi kuu England kufunga mabao matatu dhidi ya Manchester United.

Mo Salah hazuiliki?

Mmisri huyu amefunga katika mechi 10 mfululizo na moja ya msimu uliopita, likiwa goli lake la 15 katika michezo 12 tu ya mashindano mbalimbali aliyocheza msimu huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt, Salah sasa ameingia katika orodha ya wachezaji 10 duniani walioweza kufunga katika mechi 10 mfululizo katika karne ya 21, akiungana na kina Carsten Jancker (Bayern Munich) Cristiano Ronaldo (Real Madrid) Ruud van Nistelrooy (Manchester United) - 14 goals between 05/12/01 Robert Lewandowski (Bayern Munich) Ruud van Nistelrooy (Manchester United) Lionel Messi (Barcelona) na Duvan Zapata (Atalanta)

Kwa sasa Mo Salah anaongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi kuu England 10, katika michezo 9 ya msimu huu.

qq

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mo Salah (katikati) akizingirwa na mabeki wa Manchester City

Mo Salah, 29 amefikisha mabao 107 katika ligi kuu England na kuongoza waafrika waliofunga mabao mengi zaidi katika ligi hiyo, akimpiku nyota wa zamani wa Chelsea kutoka Ivory Coast, Didier Drogba aliyefunga mabao 104.

Kitu cha kipekee ni kwamba, Drogba alihitaji michezo 292 katika misimu nane ya ligi kuu kufikishsa mabao hayo, wakati Salah amefunga mabao hayo katika michezo 166 tu, mechi 153 akiichezea Liverpool, 13 akiwa na Chelsea alipofunga mabao mawili tu.

Mo Salah ni kama hakuna wa kumzuia kwa sasa, akifunga atakavyo, kwa mabao bora tena kwa timu ngumu. Salah amefunga dhidi ya Manchester United, Manchester City na Chelsea, klabu zinazoonekana kuwa bora kwenye eneo ulinzi. Wengi wanajiuliza kama timu hizi zimeshindwa kumzuia nani ataweza kumzuia?

Salah ni mchezaji bora kwa sasa duniani?

Kwa muongo mmoja uliopita ukitaja mchezaji bora duniani , ulikuwa unamtaja Lionel Messi (PSG) ama Cristiano Ronaldo(Manchester United), kutokana na kuwa na muendelezo wa viwango bora kila msimu, ingawa wapo kadhaa walioibuka kwa kufanya vyema kwenye misimu kadhaa kama Luca Modric, Thierry Henry, Robert Lewandowski na sasa Mo Salah anapita njia hizo, ikiwa ni msimu wake wa nne sasa Liverpool unakwenda akiwa kwenye kiwango bora

Yuko kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d'Or itakayotolewa Novemba 29 mwkaa huu, huku Messi akipigiwa chapuo zaidi kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya 7 baada ya mwaka 2021 kuwa mwaka mzuri kwake, akifunga mabao 40 na kutoa pasi za mabao 14 katika michezo 48 aliyozichezea Barcelona, Paris Saint-Germain na Argentina.

Akifanikiwa kutwaa kombe la 'Copa del Rey akiwa na Barcelona kabla ya kutwaa kombe la Copa Amerika akiwa na Argentina, kombe alilolisubiri katika maisha yake yote ya soka.

Hata rekodi hizi za Messi, bado Mo Salah anaonekana mshindani wa wazi katika tuzo itakayofuata ya mwaka 2022.

aasas

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Salah ni miongoni mwa waafrika wachache waliotwaa tuzo zaidi ya moja ya mchezaji bora Afrika.

Kiwango cha Salah kwa sasa, ni bora pengine kuliko wakati mwingine wowote akiwa Liverpool. Licha ya kufunga, anatengeneza pasi za kufunga ambapo katika ligi kuu mpaka sasa ametengeza pasi 5 za mabao. Kwa ujumla katika mabao 23 waliyofunga Liverpool msimu huu, Salah amehusika katika mabao 15 hiyo ni zaidi ya nusu na karibu robo tatu ya mabao yote (65%).

Ukiacha kufunga tu mabao, Salah anafunga mabao ya kiwango bora na kwa mtindo usio wa kawaida kudhihirisha uwezo na kipaji chake. Magoli dhidi ya Manchester City na Watford, yanadhihirisha uwezo wa mshambuliaji huyo anayewekwa daraja moja kwa sasa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Goli la Salah dhidi ya Manchester City kwake ni "moja ya magoli bora kabisa yaliyowahi kufungwa kwenye ligi kuu England" kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa England Alan Shearer.

Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn Chris Sutton anasema "Kwa sasa, ni bora kuliko [Lionel] Messi na [Cristiano] Ronaldo,"

Mpaka sasa amefanikiwa kutwa tuzo mbili za mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017 na 2018, akitwaa pia tuzo za mchezaji bora wa ligi kuu 2017 /2018 na mfungaji bora wa 2018 na 2019 .

0 comments:

Post a Comment