Kocha Antonio Conte amesema haamini kuwa Chelsea imefahamu namna ya kumtumia Romelu Lukaku na kudai Thomas Tuchel bado hajapata kilichobora kutoka kwa nyota huyo.
Lukaku amejiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 98 katika dirisha la usajili lililopita na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli manne kwenye michezo yake minne.
Ingawaje Conte, ambaye amewahi kufanya kazi na Lukaku wakiwa Inter Milan, anafikiri kuna mengi yanakuja kutoka kwa mshambuliaji huyo na anaamini Chelsea inahitaji kumtumia kwa njia nyingine baada ya kushindwa kufunga wakati the Blues wakipoteza kwa goli 1-0 Champions League mbele ya Juventus.
”Nadhani bado anaweza kufanya vizuri, juu ya yote na mbinu zake. Tayari ni mchezaji wa kiwango juu, lakini kwa mchezaji ni lazima aendelee kuimarika kila siku mpaka atakapostaafu.” Conte alipoiambia Sky Sport Italia.
”Kama unakuwa na mshambuliaji wa kati kama huyu, unahitaji kumtumia na sidhani kama Chelsea wameshindwa kutambua namna ya mkutumia.Endapo watafahamu namna ya kumtumia Lukaku, Chelsea inaweza kujakuwa majo ya timu yenye ushindani mkubwa Champions League msimu huu.
Msimu uliyopita, Conte aliweza kuipatia Inter ubingwa wao wa kwanza wa Serie A title baada ya miaka 10 kupitita huku Lukaku akifunga jumla ya magoli 24.
0 comments:
Post a Comment