Friday, October 1, 2021

 






Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania na Muwekezaji wa Simba SC Mo Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa thamani ya Tsh Bilioni 20 amewanyoshea kidole wanasema kaondoka na kusema huo ni upotoshaji na unatakiwa kupuuzwa.

Pia amesema kuwa yeye bado yeye ni Muwekezaji wa Simba na ataendelea kuijenga Simba kadri ya uwezo wake.

Hata hivyo Mo amewataka  mashabiki na wapenzi wa Simba  kupuuza upotoshaji unaodai amejiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kutokana na maelekezo y FCC na kusema hiyo sio kweli huku akisisitiza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na mara nyingi kutokuwa nchini

0 comments:

Post a Comment