Thursday, October 7, 2021

HISPANIA imefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mataifa Ulaya baada ya kuwachapa wenyeji, Italia mabao 2-1 usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan.

Mabao ya Hispania yote yalifungwa na mshambuliaji wa Manchester City, kinda wa umri wa miaka 21, Ferran Torres dakika ya 17 na 45 mara zote akimalizia pasi za Mikel Oyarzabal wa Real Sociedad, wakati la Italia lilifungwa na Lorenzo Pellegrini  dakika ya 83.
Ushindi huo unahitimisha rekodi ya Italia kucheza mechi 37 mfululizo bila kupoteza, lakini pia kikosi cha  Luis Enrique kimelipa kisasi cha kutolewa na Azzuri kwenye Nusu Fainali ya Euro 2020 kwa penalti.


Hispania sasa itamenyana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine leo kati ya Ubelgiji na Ufaransa Uwanja wa Allianz Jijini Torino.

0 comments:

Post a Comment