KLABU ya Azam FC imewasimamisha wachezaji wake watatu, beki na Nahodha, Aggrey Morris pamoja na Wasaidizi wake, viungo Salum Abubakar 'Sure Boy' na Mudathir Yahya kwa kile kilichoelezwa makosa ya utovu wa nidhamu.
Taarifa ya Azam FC iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Thabit Zacharia imesema watatu kwa pamoja walimtolea maneno yasiyofaa Meneja wa timu hiyo, Luckson Kakolaki.
0 comments:
Post a Comment