Friday, October 15, 2021



HAJI Manara aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Simba na sasa ni Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa ameandaa mawakiki 10 wa kusimamia kesi yake na Simba.

Manara amebainisha kuwa yupo kwenye mpango wa kuishtaki klabu hiyo kwa madai ya kumfanyia dhuluma na akitaka kulipwa stahiki zake kwa muda wa miaka 6.

Ofisa huyo ambaye yupo kwenye kipengele cha kuwania tuzo kwa muhamasishaji bora kwa msimu wa 2020/21 ambao alikuwa Simba amesema kuwa hatakubali kuona jasho lake linapotea.

"Nitaenda mahakamani kudai haki yangu, nawadai Simba pesa nyingi wamenitumia miaka zaidi ya sita.

"Nimefanyiwa dhuluma, hawa sio binadamu kwa kweli mimi nina kifua sijawahi kusema ila siku nikisema mtanielewa, kisa umaarufu eti mimi ananichukia.

"Na iliwauma zaidi mimi kwenda Yanga,walinifanyia mambo mengi mabaya na nitadai haki yangu nimeandaa mawakili 10," alisema Manara

0 comments:

Post a Comment