Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Blackburn, Chris Sutton amesema kuwa nyota wa Liverpool, Mohamed Salah ni mshambuliaji bora kwa sasa kuliko Messi na Ronaldo.
“Kwa sasa, ni bora kuliko [Lionel] Messi na [Cristiano] Ronaldo,” amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Blackburn, Chris Sutton
Wakati, Alan Shearer kwa upande wake amedai kuwa goli la Mo Salah dhidi ya Manchester City ni moja kati ya bao bora kabisa yaliyowahi kufungwa Ligi Kuu nchini Uingereza.
Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 29, mpaka sasa ameshafunga jumla ya magoli tisa (9) kwenye michezo yake tisa (9) msimu huu.
0 comments:
Post a Comment