Liverpool wanafuatilia kwa karibu hali ya Ousmane Dembele huko Barcelona. Mkataba wa winga huyo wa Ufaransa wa miaka 24, ambaye hajacheza tangu Euro 2020 kutokana na jeraha la goti unamalizika mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Chelsea wamefanya mazungumzo rasmi na Real Madrid juu ya kumsajili tena mchezaji nyota wa Ubelgiji Eden Hazard,34 - lakini klabu hiyo ya Uhispania inataka Reece James, 21, kuwa sehemu ya makubaliano yatakayofikiwa. (El Nacional - in Catalan)
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre, 63, na kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard, 43, wanatajwa sana na wamiliki wapya wa Newcastle United ambao wangelipendelea mmoja wao achukue nafasi ya Steve Bruce katika uwanja wa St James' Park. (Telegraph -usajili unahitajika)
Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana nia ya kusaini mkataba mpya na Gunners wakati mkataba wake wa sasa utakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Football.London)
Kiungo wa Wales Aaron Ramsey, 30, bado anaamini anaweza kufanikiwa Juventus akiwa amesalia na msimu mmoja na nusu katika mkataba wake wa sasa. (Times - subscription required)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, anasema "hajafurahia vilivyo" Paris St-Germain - miezi minne tu baada ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Liverpool. (Independent)
Klabu Feyenoord ya Uholanzi inajiandaa kuwasilisha upya dau la kumnunua winga wa Manchester United na Ivory Coast Amad Diallo, 19, baada ya jeraha alilokuwa nalo kuvuruga uhamisho wake wa mkopo msimu wa joto. (Sun)
Manchester United huenda wakamuuza kiungo wa kati mshambuliaji Jesse Lingard, 28, kwa kima cha pauni milioni 15 mwezi Januari ikiwa hatasaini mkataba mpya Old Trafford, kwani kandarasi ya sasa inakamilika msimu ujao. (Sun)
Juventus wameanzisha mazungumzo na ajenti wa Donny van de Beek, 24, wa Manchester United, kwa lengo la kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uholanzi. (La Stampa via Football Italia)
Juventus pia wanajiandaa kumsajili kwa mkopo nyota wa Manchester City na Portugal Bernardo Silva, 27, mwezi Januari mwakani. (Calciomercato - in Italian)
Muingereza Ben Davies, 26, anaamini kuwa ataendelea kuwa Liverpool licha ya kutopata muda wa kuchezea klabu hiyo tangu alipojiunga nayo Februari na kisha kwenda Sheffield United kwa mkopo wa msimu mzima. (Liverpool Echo)
Kipa wa Uhispania David Raya, 26, amesema anafurahia kuwa Brentford licha ya kunyatiwa na Arsenal na Everton. (Cadena Ser - in Spanish)
0 comments:
Post a Comment