Thursday, November 4, 2021

 



WENYEJI, Real Madrid wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Shakhtar katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
Mabao ya Real Madrid yamefungwa na mshambuliaji mkongwe Mfaransa, Karim Benzema dakika ya 14 na 61, wakati la Shakhtar limefungwa na Fernando dakika ya 39.
Real Madrid inafikisha pointi tisa na kupanda kileleni mwa Kundi hilo ikiizidi pointi mbili Inter Milan, wakati Shakhtar inashika mkia hadi sasa ikiwa na pointi moja tu nyuma ya Sheriff yenye pointi sita baada ya wote kucheza mechi nne.

0 comments:

Post a Comment