Newcastle inapanga kutangaza kocha wao mpya wiki hii, huku kocha wa zamani wa Arsenal alijejiunga na Villarreal Unai Emery, 49, akionekana kuwa kocha mwenye uwezo wa kuifunza klabu hiyo .. (Mirror)
Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vitano vilivyotoa ofa kumsajili kiungo mshambuliaji Marco Asensio, 25, kutoka Real Madrid mwezi Januari, sambamba na Juventus, AC Milan na Borussia Dortmund. (El Nacional - in Spanish)
Antonio Conte anajiandaa kutia saini mkataba wa pauni milioni 20 kama kocha wa Tottenham, huku wachezaji wa Spurs wakiwa tayari kwa kocha wa zamani wa Chelsea na Inter Milan, kuungana naye Jumanne. (Telegraph - subscription required)
Newcastle inapanga kutangaza kocha wao mpya wiki hii, huku kocha wa zamani wa Arsenal alijejiunga na Villarreal Unai Emery, 49, akiibuka kuwa mshindani hivi karibuni. (Mirror)
Aston Villa wamefanya mawasiliano yasiyo rasmi na kocha wa zamani wa Roma Paulo Fonseca wakati klabu hiyo ikimfikiria kujaza nafasi ya Dean Smith. (Mail)
Al Sadd amewaambia maafisa wa Barcelona kuwa watakwenda Qatar kuridhia makubaliano kwa ajili ya Xavi, 41, kuchukua mikoba ya ukufunzi kwenye klabu hiyo aliyowahi kuichezea. (AS - in Spanish)
Conte amemuomba mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy fungu la bajeti la karibu pauni milioni 237 kwa ajili ya kuwanunua wachezaji wa ligi ya Serie A aliowabainisha. (Calciomercato, via Express)
Xavi ameipatia Barcelona orodha ya wachezaji wanne anaotaka kuwasajili, ikiwemo kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba,28, ambaye mkataba wake utakamilika mwishoni mwa msimu huu. (El Nacional - in Spanish)
Tottenham wanajiandaa kumlipa Nuno Espirito Santo kitita cha pauni milioni14- lakini kipengele cha mkataba wa kocha huyo wa kireno kingeruhusu Spurs kumfukuza bila malipo mwishoni mwa msimu kama angeshindwa kumaliza ligi ya primia katika nafasi sita za juu. (Sun)
AC Milan wanajiandaa kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic,40, ofa hii ni ongezeko la mkataba kwa makubaliano yaleyale ya mkataba wa sasa.(Calciomercato - in Italian)
Arsenal wanafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Torino, Muitaliano Andrea Belotti,27. (Calciomercato)
Arsenal watatoa ofa kumsajili mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic,23, kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Express)
Juventus huenda wakalazimika kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey,30 au kiungo wa kati wa Kimarekani Weston McKennie,23, kwa ajili ya kupata fedha za uhamisho wa mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic,21 na kiungo wa kati wa Ubelgiji Axel Witsel,32. (Tuttosport - in Italian)
Paris St-Germain wanafikiria kufuta kandarasi ya miaka miwili ya beki wa Uhispania Sergio Ramos, 35, ambaye alijiunga kwa uhamisho huru kutoka Real Madrid mwezi Julai lakini bado hajaichezea klabu hiyo ya Ufaransa.(Le Parisien, via AS)
PSG wanajiandaa kwa ofa ya kumnasa mlinzi wa Kiungo mkabaji Joao Palhinha,26, anayekipiga Sporting Lisbon. (O Jogo - in Portuguese)
0 comments:
Post a Comment