Manchester United hawana mpango wa kumpa ofa Cristiano Ronaldo, 36, ya kuwa kocha katika klabu hiyo baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa ana mpango wa kuchukua jukumu hilo atakapostaafu. (Star)
Mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 22, amesema ''ana furaha sana'' katika klabu ya Uhispania ya Sociedad lakini ''siku moja itakuwa vizuri kucheza England''. (Independent)
Kocha wa Roma Jose Mourinho amebainisha kuwa viungo wa Kiingereza Loftus-Cheek wa Clesea na Harry Winks wa Tottenham ni wachezaji anaowalenga. (Corriere dello Sport, in Italian)
Inter Milan wako tayari kumzuia meneja wa zamani na mkufunzi mpya wa Tottenham Antonio Conte kusajili wachezaji wowote kutoka kwao, huku mkurugenzi wa timu hiyo ya Serie A Piero Ausilio akisema "hatutazingatia uwezekano wowote wa uhamisho kutoka kwetu" mnamo Januari.(Sky Italia, via Express)
Newcastle United wanataka kumchukua kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi mwenye umri wa miaka 22 kutoka Marseille, ambapo kwa sasa yuko kwa mkopo kutoka Arsenal.(Mirror via Foot Mercato)
Southampton, pamoja na Monaco na vilabu kadhaa vya Bundesliga, wanamfuatilia mshambuliaji wa Austria , mzaliwa wa Nigeria anayecheza Red Bull Salzburg Chukwubuike Adamu, 20. (Mail)
Liverpool wana uhakika wa kuvishinda vilabu kadhaa kwenye usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Fabio Carvalho, huku kandarasi ya winga huyo mwenye umri wa miaka 19 na Fulham ikimalizika msimu ujao wa joto. (Teamtalk)
Mlinzi wa Japan Takehiro Tomiyasu, 22, anasema alikaribia kujiunga na Tottenham kabla ya kusaini kwa wapinzani wao wa London kaskazini Arsenal msimu wa joto.(DAZN Japan, via Goal)
Atletico Madrid wanapanga kumpa mkataba kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, 28, ambaye mkataba wake na Inter Milan utamalizika msimu ujao wa joto na amekuwa akihusishwa na Manchester United na Newcastle. (Fichajes - in Spanish)
Barnsley, Derby County, Millwall na Luton Town ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili winga Muingereza Jack Clarke mwenye umri wa miaka 20 kutoka Tottenham mwezi Januari. (Teamtalk)
0 comments:
Post a Comment