Kocha Mkuu wa klabuya Namungo, Hemed Selemani ‘Morocco’ amemtupia lawama mwamuzi wa kati Nassoro Mwinchui kwa kudai kuwa amechangia timu yake kupoteza bao 1-0 dhidi ya Simba SC usiku wa jana kwenye dimba la Mkapa.
Morocco ameyasema hayo wakati alipoulizwa swali na Mchambuzi wa Michezo wa EATV & Radio, Abissay Stephen JR kwenye mahojiano na Wanahabari yaliyofanyika muda mchache tu baada ya mcheoz huo wa ligi kuu kumalizika.
Morocco amesema:
"Lakini me naona leo mechi ya mwamuzi. Mechi ya mwamuzi, yeye ndiyo kaamua. 90+5 nafikiri tumefungwa 90+4 after all game imeisha, kulikuwa na so many incidents ambazo pia zilikuwa zinawezekana kutu-favour sisi ambazo hakuzionesha" Amesema Morocco.
Mbali na lawama hizo kwa mwamuzi, Lakini amekiri kuwa hali ya wachezaji wake hususani wa eneo la Ulinzi kupoteza umakini umepelekea kuwa wahanga wakufungwa mabao dakika chache kabisa kabla mchezo haujamalizika.
Namungo ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 5 baada ya kucheza michezo 5, ikifungwa 2, sare 2 na kushinda 1 pekee.
0 comments:
Post a Comment