TANZANIA leo imepoteza mechi ya pili mfululizo kwenye michuano ya CECAFA wanawake U20 baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Uganda Uwanja wa FTC Njeru.
Kipigo hicho kinafuatia kipigo cha 2-1 kutoka kwa Ethiopia kwenye mchezo uliopita.
Mechi mbili za awali, Tanzanite ilishinda 1-0 dhidi ya Eritrea na 3-2 dhidi ya Burundi na itashuka tena dimbani Jumanne kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti.
0 comments:
Post a Comment