Thursday, November 4, 2021



KLABU ya Liverpool imefanikiwa kutinga Hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa Kundi B usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield.
Mabao ya Liverpool katika mchezo ambao wageni, Atletico Madrid walimaliza pungufu kufuatia Felipe kutolewa kwa kadi nyekundu yamefungwa na Mreno Diogo Jota dakika ya 13 na Msenegal, Sadio Mane dakika ya 21.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 12 na kujihakikishia kusonga mbele ikiendelea kuongoza Kundi kwa pointi saba zaidi ya Porto wanaofuatia, wakati Atletico Madrid inabaki na pointi nne mbele ya AC Milan inayoshika mkia kwa pointi yake moja baada ya mechi nne kila timu.

0 comments:

Post a Comment