Thursday, November 4, 2021

 

Philippe Coutinho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Newcastle wanatarajiwa kumsajili mchezaji wa zamani wa Liverpool, kiungo wa kati Philippe Coutinho, huku Barcelona wakitamani kumuuza mchezaji huyo,29. (Sport)

Manchester United wanapanga kumfuatilia kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, huku wakiongeza kasi ya kutafuta mbadala wa nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 28. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe anaweza kutaka kipengele cha Olimpiki kiingizwe katika mkataba wowote unaowezekana na Real Madrid baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kueleza hadharani nia yake ya kuiwakilisha Ufaransa kwenye Michezo ya Paris mnamo 2024. (AS-in Spanish)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Klabu ya Palmeiras ya Brazil inapenda kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavani,34, mkataba wa mchezaji huyo wa Uruguay utakapokwisha majira ya joto yajayo. (Daily Express)

Kocha wa Villrreal Unai Emery,50, ametupilia mbali ofa ya uhamisho kwenda Newcastle kwasababu klabu hiyo imetaka kiwepo kipengele kwenye mkataba wake kitakachowaruhusu kumtimua ikiwa watashuka daraja mwishoni mwa msimu. (Daily Mirror)

Machester City wamemwambia kocha wa Leicester Brendan Rodgers,48, kuwa wangependa achukue mikoba ya Pep Guardiola Mhispania huyo mwenye miaka 50 atakapoachhana na mabingwa hao wa ligi ya Primia. (The Transfer Podcast via Leicester Mercury)

Brendan Rodgers

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham wanaongoza kinyang'anyiro cha kumnasa mhambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, huku Mserbia huyo akiwa tayari kuhamia ligi ya Primia. (La Nazione - in Italian)

Barcelona wana matumaini ya kumshikilia winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, mkataba mpya wa miaka mitatu ifikapo mwishoni mwa Novemba. Dembele, ambaye mkataba wake wa sasa unaisha msimu ujao wa joto, inasemekana amekubali kukatwa mshahara.(Mundo Deportivo - in Spanish)

Everton wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Real Mallorca na Ghana Iddrisu Baba, 25, mwezi Januari.(Fichajes via Daily Mail)

Ousmane Dembele

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wolves wanapanga "kuharakisha mazungumzo" na RB Leipzig ili kubadilisha mkopo wa mshambuliaji wa Korea Kusini Hwang Hee-chan wa miaka 25 kuwa mkataba wa kudumu. Klabu hiyo ya Midlands pia inaweza kufufua majaribio yao ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ureno Renato Sanches, 24, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lille. (Birmingham Mail)

Barcelona watamchukua kiungo wa kati wa Tottenham mwenye umri wa miaka 24 Tanguy Ndombele mwezi Januari, lakini wanaweza tu kumudu mkataba wa mkopo kwa Mfaransa huyo. (Sport - in Spanish)

Mkurugenzi wa kandanda wa Liverpool Michael Edwards, kiungo muhimu katika mafanikio ya hivi majuzi ya Wekundu hao na mhimili mkubwa katika kusajili mastaa kama Mohamed Salah na Virgil van Dijk, anaweza kuhamia RB Leipzig ya Ujerumani mwezi Januari.(Sport Bild via Daily Mail)

0 comments:

Post a Comment