Saturday, January 15, 2022

 


Mondher Kebaier (right) remonstrates with officials

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kocha wa Tunisia Mondher Kebaier akimuonesha muamuzi kuwa mechi imeisha kabla ya muda

Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) limetupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) kuhusu mchezo wao na Mali kumalizika mapema, sekunde 13 kabla ya muda wa mechi kuisha.

Katika taarifa iliyotolewa, Caf ilisema kamati ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika ilikutana siku ya Alhamisi na kukataa maandamano hayo lakini haikutoa maelezo zaidi.

Caf pia ilithibitisha matokeo ya mchezo wa Jumatano kama ushindi wa 1-0 dhidi ya Mali, bao ambalo mwamuzi wa Zambia Janny Sikazwe, alisema alipigwa na jua, alipuliza mapema.

Tayari alikuwa amepiga filimbi ya kumaliza muda wa mechi baada ya dakika 85, na kugundua makosa yake hivyo kuendelea na mechi.

Mapema siku ya Alhamisi, afisa wa FTF Hussein Jenaieh alilisisitiza kuwa: "Tutafanya chochote kinachohitajika ili kutetea haki za timu ya taifa. Sisi sio watoto."

Afisa wa habari wa FTF Kais Reguez alikataa kuelezea kwa undani alipoulizwa kuhusu chanzo cha malalamiko ya Tunisia, ambayo alithibitisha.

Mwamuzi wa mchezo huo, Sikazwe, inasemekana alilazimika kwenda hospitali kupata nafuu baada ya mchezo kumalizika, na ndiyo maana afisa wa nne alipewa jukumu la kutaka kuanza tena mchezo kwa dakika 20 baada ya kushindwa.

Wakati Mali walijitokeza, Tunisia hawakutokea, kwani baadhi ya wachezaji wao walikuwa wakipooza miili yao kwa barafu .

"Mwamuzi alipigwa na jua, jambo ambalo liliathiri maamuzi yake katika mchezo," afisa mwamuzi wa Caf Essam Abdul Fattah aliambia vyombo vya habari vya Misri. "Baada ya mchezo, alihitaji kwenda hospitali kwa sababu hali ya hewa ilikuwa ya joto."

Baada ya sare ya 0-0 ambayo haikutarajiwa dhidi ya Sierra Leone, mabingwa watetezi Algeria walilaumu kuonesha kwao kutokana na joto nchini Cameroon.

Tunisia, mabingwa wa 2004, waliingia dimbani wakijua kwamba timu changa na mahiri ya Mali huenda ikawa washindani wao wakuu kundini.

Wakiwa dakika za mwisho , zikiwa zimesalia dakika tano tu za kumaliza mchezo, walipigwa na butwaa wakati mwamuzi Sikazwe alipopuliza kipyenga.

Mzambia huyo baadaye aliangalia muda wake na kuendelea na mchezo, huku akimtoa mchezaji wa Mali kwa kadi nyekundu, kisha akalipua na saa kuonyesha dakika 89 na sekunde 47.

Katika hali isiyo ya kawaida, mkutano wa waandishi wa habari wa 'baada ya mechi' wa kocha huyo wa Mali ulikatizwa huku ikitangazwa kwamba mchezo huo ungetakiwa kuanza upya kwa dakika tisini, jambo ambalo halikufanyika.

"Walituomba turudi uwanjani, hatukujua - hatukujua kilichokuwa kikiendelea," mlinzi wa Tunisia Bilel Ifa aliwaambia waandishi wa habari.

"Tunatumai mechi itarudiwa. Mwamuzi hakujua kilichokuwa kikiendelea tangu mwanzo wa mchezo."

Kocha msaidizi wa Tunisia alikasirishwa na tukio hilo na uwezekano wa uharibifu wake wa sifa kwa mchezo wa Afrika.

"Kwa bahati mbaya, hatuwezi kuona mambo kama haya katika kiwango hiki cha juu barani Afrika - Soka la Afrika haliwezi kusonga mbele hivi," kocha msaidizi wa Tunisia Jalel Kadri aliwaambia wanahabari.

"Mwamuzi "alitikiswa" leo. Alisita hata kumtazama Video Assistant Referee (VAR), hakujua hata jinsi ya kufika kwenye VAR."

0 comments:

Post a Comment