PAMOJA na kucheza pungufu, Arsenal imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England usiku huu Uwanja wa Anfield.
Arsenal walilazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 24 baada ya Granit Xhaka kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Diogo Jota.
Liverpool sasa itasafiri kwenda London kwa mchezo wa marudiano Januari 20 Uwanja wa Emirates na mshindi wa jumla atakutana na Chelsea katika fainali ambayo imeitoa Tottenham kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 2-0 Stamford Bridge na 1-0 Tottenham
0 comments:
Post a Comment