MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Romelu Lukaku ameweka wazi kuwa kwa sasa hana furaha ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel.
Jambo hilo ni kubwa na gumu kwa kuwa linaweza kuvuruga mwendo wa kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.
Nyota huyo ameweka wazi kwamba anahitaji kuweza kurejea Inter Milan ili akaendelee na maisha yake kama ilivyo kawaida zamani tofauti na sasa.
Ikumbukwe kwamba raia huyo wa Ubelgiji alisajiliwa kwa pauni 97.5 milioni na alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokunja mkwanja mrefu kipindi cha usajili.
Kupitia Sky Sport Italy, amesema:”nipo fiti lakini sina furaha na hali iliyopo Chelsea. Tuchel amechagua kucheza na mfumo mwingine.
“Sitaka tamaa, nitakuwa mweledi. Sina furaha na hali ilivyo lakini mimi ni mweledi na siwezi kukata tamaa sasa,”.
0 comments:
Post a Comment