Sunday, January 2, 2022

 



MABINGWA watetezi, Manchester City wametanua uongozi wao hadi pointi 11 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Riyad Mahrez dakika ya 57 kwa penalti baada ya 
Granit Xhaka kumchezea rafu Bernardo Silva na Rodri dakika ya 90 na ushei kufuatia Arsenal kutangulia kwa bao la Bukayo Saka dakika ya 31.
Kwa ushindi huo katika mchezo wa 21, Man City inafikisha pointi 53 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 11 zaidi ya   Chelsea iliyocheza mechi 29.
Arsenal waliomaliza pungufu baada ya Gabriel kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 59 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Gabriel Jesus wanabaki na pointi zao 35 za mechi 20 katika nafasi ya nne.

0 comments:

Post a Comment