Sunday, January 2, 2022

 



TIMU ya DTB imeendeleza wimbi la ushindi katika ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao, ijulikanayo kama Championship baada ya kuwachapa wenyeji, Pamba SC 1-0 jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao pekee la DTB leo limefungwa na mshambuliaji Mghana, Nicholas Gyan dakika ya 57 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 33 na kuendelea kuongoza Championship kwa pointi nne zaidi ya Ihefu SC baada ya wote kucheza mechi 13.
Jahazi la Pamba linazidi kuzama, sasa wakibaki na pointi zao 16 za mechi ya 13 katika nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu16 na sasa badala ya kuwania kupanda Ligi Kuu, wanahitaji kupambana wasishuke.



0 comments:

Post a Comment