Divock Origi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Divock Origi akishangilia kufunga bao la dakikika ya mwisho

Mkurugenzi wa michezo wa Lazio Igli Tare ameanzisha mazungumzo na Liverpool kumhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, huku Reds wakiwa tayari kumuuza nyota huyo wa miaka 26 kwa kuhofia kumpoteza kwa uhamisho wa bure mwezi Juni. (LazioNews24 - in Italian)

Manchester United wamedhamiria kumsajili kiungi wa Wolverhampton Wanderers na Ureno Ruben Neves, 24,mwezi huu. (The Sun)

Mkufunzi wa Aston Villa Steven Gerrard amempigia simu binafsi kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, ambaye alicheza naye Liverpool, kuhusu uwezekano wa Mbrazil huyo wa miaka 29 kuhamia Villa Park kwa mkopo. (El Partidazo de Cope, via Mirror)

Philippe Coutinho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Coutinho(kulia) aliondoka Liverpool na kujiunga na Barcelona kwa mkataba wa £142m 2018

Liverpool huenda ikamruhusu mlinzi wa Wales Neco Williams, 20, na beki wa Muingereza Nathaniel Phillips, 24, kuondoka klabu hiyo katika dirisha la uhamisho wa Januari. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 31, anajiandaa kuondoka Juventus, ambako analipwa euro 325,000 kwa wiki. (Sky Sports)

Kiungo wa Everton Lucas Digne, 28, huenda akahamia klabu nyingine ya Ligi ya Primia. Hata hivyo Newcastle sio chaguo la mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (Fabrizio Romano via Twitter)

Lucas Digne and Rafael Benitez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumnunua beki wa Barcelona na Marekani Sergino Dest, 21, kama mbadala wa Digne. (Daily Star)

Newcastle wamepewa beki wa Ufaransa Samuel Umtiti 28, na Barcelona kwa mkataba wa bure na chaguo la kumnunua. (Daily Mail)

Aston Villa hawana 'nafasi' ya kumsajili kiungo wa Liverpool na Uingereza Joe Gomez. (Athletic - subscription required)

Borussia Dortmund watafanya uamuzi kuhusu hatma ya mshambuliaji wa Norway wa miaka 21 Erling Braut Haaland 'wiki chache zijazo'. (Daily Mail)

Erling Braut Haaland

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Borussia Dortmund kuamua hatma ya mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland

West Ham wamewasilisha dau la pauni milioni tano kumnunua kwa mkopo mshambuiaji wa Flamengo Mbrazil Gabriel Barbosa, 25, hadi Disemba 2023. (Sport - in Spanish)

Hadi wachezaji 11 wanatarajiwa kuondoka Manchester United, baada ya kukatishwa tamaa na maisha ya Old Trafford na fununu za mgogoro wa chumba cha kubadilishia nguo. (Mirror)

Manchester United wanajaribu kumsajili mlinzi wa Ufaransa Dan-Axel Zagadou, 22, ambaye yuko huru kuondoka kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Borussia Dortmund. (Foot Mercato - in French)