Aston Villa wamekubali kumnunua kiungo wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho kwa mkopo kutoka Barcelona hadi mwisho wa msimu huu.
Mkataba huo, ambao unategemea matibabu na kibali cha kazi kutolewa, ni pamoja na chaguo la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 29.
Coutinho alijiunga na Barcelona kwa uhamisho wa £142m kutoka Liverpool Januari 2018.
Hata hivyo, hajapata matokeo yaliyotarajiwa na Barca wanataka kumsogeza ili kupunguza bili yao ya mshahara.
Arsenal, Everton, Newcastle na Tottenham pia walihusishwa kutaka kumnunua Coutinho.
Mchezaji huyo, ambaye amefunga mabao 26 katika mechi 106 alizochezea Wacatalunya hao, ana miezi 18 kukamilisha mkataba wake wa Nou Camp, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2022-23.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, huenda akaondoka Manchester United msimu huu wa joto ikiwa hataridhika na chaguo la klabu hiyo la kocha wa kudumu. (Star)
Liverpool wanakaribia kufikia mkataba wa kima cha pauni milioni 60 kumsajili winga wa Colombia Luis Diaz, 24, kutoka Porto. (Sun)
Mshambuliaji wa Liverpool Mbelgiji Divock Origi, 26, na mshambuliaji wa Bournemouth wa miaka 24-Muingereza Dominic Solanke ni miongoni mwa wachezaji wanaonyatiwa na Newcastle wanapotafuta kujaza pengo lililoachwa na Callum Wilson aliyejeruhiwa. (Telegraph - subscription required)
Newcastle wamekataa dao la Everton la kumnunua Sean Longstaff. Mkataba wa kiungo huyo wa miaka 24-unakamilika mwisho wa msimu huu lakini Magpies wana matumaini ya kufikia mkataba mpya na kiungo huyo wa kati wa Uingereza. (Shields Gazzette)
Newcastle na klabu zingine za Ligi ya Primia zinapania kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Todd Cantwell, 23. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino yuko tayari kupokea ofa yoyote ya kuwa kocha wa Manchester United. (Sun)
Tottenham wako tayari kufufua mpango mpya wa kumsaka winga wa Uhispania na Wolves Adama Traore, 25. (Athletic - subscription required)
Chelsea haiko tayari kulipa ada inayohitajika kumfanya kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo Saul Niguez, 27, kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu kutoka Atletico Madrid. (Express)
Manchester United hawana mpango wa kufanya usajili wowote mwezi huu lakini watamtafuta kiungo wa kati msimu wa joto, huku mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 Declan Rice akipigiwa upato kujiunga nao. (Mchezo)
Arsenal wametoa ofa ya mchezaji zaidi ya pesa kumnunua mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, 21.(Ben Jacobs - CBS)
Watford wamewasilisha ombi la kutaka kumnunua beki wa kati wa Liverpool Muingereza Nathaniel Phillips, 24, ambaye ameambiwa anaweza kuondoka kwa Reds mwezi huu. (Football Insider)
Barcelona wanatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 26, kwa lengo kumsajili kwa mkataba wa kudumu kungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwisho wa msimu. (Sport - in Spanish)
Barca pia wanamyatia mlinzi wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Everton na Newcastle wameungana na Arsenal katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa wa Lyon Mbrazil Bruno Guimaraes,24. (Standard)
0 comments:
Post a Comment