Tuesday, January 18, 2022

 

Anthony Martial

HANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mkataba wa Anthony Martial katika klabu ya Manchester United inaendelea hadi 2024

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26, anataka kuondoka Manchester United lakini sio kwa mkopo kwenda klabu nyingine ya Uingereza. Barcelona, Sevilla na Juventus ndio klabu tatu anazopigiwa upato kujiunga nazo katika uhamisho wa Januari. (Fabrizio Romano)

Manchester United wanamnyatia kiungo wa kati wa Aston Villa na Scotland John McGinn, 27, katika uhamisho wa msimu wa joto. (Telegraph - subscription required)

Beki wa Rangers Borna Barisic, 29, amethibitisha kuwa kuna klabu iliyowasilisha ombi la kumnunua awali katika dirisha la uhamisho, licha ya tetesi zinazomhusisha kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia na Watford na Aston Villa. (Sky Sports)

Borna Barisic

CHANZO CHA PICHA,ROB CASEY - SNS GROUP

Maelezo ya picha,

Beki wa Rangers Borna Barisic

Mazungumzo ya Arsenal na Juventus kuhusu mkataba wa mkopo wa kiungo Arthur Melo yamekwama kwa sababu klabu hiyo ya Serie A bado haijapata mbadala wa Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25.(Tuttomercatoweb, via Express)

Chelsea huenda ikapewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, huku Manchester United wakielekeza darubini yao kwa liungo wa RB Leipzig na Mali Amadou Haidara, 23, na kiungo wa Borussia Monchengladbach na Uswizi mwenye umri wa miaka 25- Denis Zakaria. (football.london)

Diego Costa, ambaye amehusishwa na Arsenal, inataka kuhamia klabu ya Brazil ya Corinthians, ambako kiungo huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 33-huenda akaungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea- Willian. (Evening Standard)

Diego Costa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Diego Costa, ambaye amehusishwa na Arsenal, inataka kuhamia klabu ya Brazil ya Corinthians

Manchester United wanaongoza Juventus na Inter Milan katika mbio za kumska kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 26, kutoka Lazio, lakini Klabu hiyo ya Serie A club huenda ikaitisha hadi angalau euro milioni 80 (£66.8m). (Il Messaggero via Sport Witness)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard anayaka kuondoka Real Madrid, lakini hana mpango wa kujiunga na Newcastle, ambao walikuwa wamewasilisha dau la £41.3m kumnunua mchezaji huyo wa miaka 31. (El Nacional - in Catalan)

Dembelle
Maelezo ya picha,

Ousmane Dembele amepewa makataa ya saa 48 kuamua kuhusu mkataba mpya aliyopewa na Barcelona

Barcelona imempatia winga wa Ufaransa wa miaka 24- Ousmane Dembele makataa ya saa 48 kuamua kuhusu mkataba mpya aliyopewa na klabu hiyo wakati mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Paris St-Germain wamewapatia Chelsea nafasi ya kumsajili mlinzi wa Ufaransa Layvin Kurzawa, lakini mkufunzi wa The Blues Thomas Tuchel hamtaki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 licha ya kumpoteza beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell, 25, kutokana na jeraha baya la goti. (Goal)

Mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 35, anakaribia kurefusha mkataba wake na Tottenham. (football.london)

Layvin Kurzawa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Chelsea wapewa nafasi na PSG kumsajili mlinzi wa Ufaransa Layvin Kurzawa(fulana ya bluu)

Demirspor ya Uturuki, anatarajiwa kujiunga na Galatasaray mwishoni mwa msimu huu. (Koha Net, via City Xtra)

0 comments:

Post a Comment