Saturday, January 1, 2022



VINARA, Yanga SC wamefunga mwaka ushindi wa kishindo wa 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkala Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Wakongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 42, Jesus Ducapel Moloko dakika ya 57, Justin Billary aliyejifunga dakika ya 71 na kiungo Mganda dakika ya 81.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 11, nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC wanaofuatia ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao 16 za mechi 11 pia katika nafasi ya sita.

0 comments:

Post a Comment