Nyota Mbrazil wa Barcelona, Neymar anakaribia kuhamia Paris Saint-Germain kwa ada ya Pauni Milioni 198 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
NYOTA
Mbrazil wa Barcelona, Neymar amewasili Jijini Paris kukamilisha
uhamisho wake klabu ya Paris Saint-Germain kwa dau la rekodi ya dunia,
Pauni Milioni 198.
Neymar
anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho ya
Pauni Milioni 596,000 kwa wiki baada ya kodi na dau la kusaini mkataba
Pauni Milioni 45.
Kwa ujumla, dili zima litaigharimu PSG kiasi cha Pauni Milioni 398.
Tetesi
za Neymar kuondoka Barcelona zilianza kuvunja taratibu kwenye vyombo
vya Habari, ingawa mwanzoni klabu ya Hispania ilikanusha na kusema
mchezaji huyo hataondoka.
Lakini hawakujua kama kulikuwa kuna mazungumzo ya siri kati ya baba yake Neymar na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi aliyekuwa akimtafutia mkataba mpya mwanawe.
Lakini hawakujua kama kulikuwa kuna mazungumzo ya siri kati ya baba yake Neymar na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi aliyekuwa akimtafutia mkataba mpya mwanawe.
Lakini
Jumatano asubuhi mambo yakaanza kuwa hadharani, baada ya Neymar kwenda
kwenye mazoezi ya Barcelona na kutumia dakika 40 kukutana na Wakurugenzi
wa klabu na kuwaaga wachezaji wenzake.
Kisha
Barcelona ikatoa taarifa muda wa chakula cha mchana ikithibitisha
kwamba Neymar ameomba kuondoka ili akakamilishe uhamisho wake PSG.
Jumatano
usiku, wakala Wagner Ribeiro, ambaye anafanya kazi za mikataba ya
Neymar, akathibitisha ada italipwa ndani ya saa 48 zijazo na mchezaji
anaweza kutambulishwa mjini Paris mapema Ijumaa.
Hakukuwa
na hotuba ya maana wakati Neymar anaaga kwenye chumba cha kubadilishia
nguo, zaidi ya kuagana na wachezaji wenzake mmoja baada ya mwingine.
Baadaye nyota mkubwa zaidi wa klabu hiyo, Muargentina Lionel Messi akaposti kwenye mtandao wa kijamii: "Ilikuwa babu kubwa kuwa nawe rafiki yangu Neymar kwa miaka yote hiyo. Nakutakia bahati nzuri katika hatua nyingine kwenye maisha yako,".

Yote haya yanatokea miezi 10 tu tangu Neymar asaini mkataba mpya wa kuendelea kucheza Barcelona hadi mwaka 2021.
Barcelona
ilithibitisha haikumpa baba yake Neymar 'cha juu' wakati wa kusaini
mkataba huo mpya, licha ya malipo ya Pauni Milioni 22 kufanywa Jumatatu
na klabu hiyo inatarajia kufuata ushauri wa kisheria baada ya uhamisho
wa mchezaji huyo kukamilika ili kujua kama malipo zaidi na wao
watatakiwa kufanya.

0 comments:
Post a Comment