
Twitter
Ukiacha North Derby iliyopigwa mchana wa leo, usiku huu
kulikuwa na Derby nyingine ya mji wa Madrid ambapo Atletico Madrid
wakiwa nyumbani waliikaribisha Real Madrid.

Dakika
90 za mchezo huu zilimalizika kwa Atletico na Real kugawana alama baada
ya mchezo huo kutokuwa na mbabe kwa kumalizika kwa sare ya bila
kufungana matokeo yanayowafanya wote kubaki na alama 24.
Wakati Derby hiyo ikipigwa pale Hispania, kule nchini Italia kulikuwa
na mchezo mkubwa kati ligi ya Serie A ambapo Ac Millan walikwenda
kuikabili Napoli.

Milan
wameambulia kipigo cha mabao mawili kwa mabao ya Lorenzo Isgne pamona
na lile la Piotos Zielinski huku la Millan likiwekwa kimiani na Aressio
Romagnoli.
Baada ya mchezo wa leo Sc Napoli wanazidi kujikita kileleni mwa ligi
ya Serie A wakiwa na alama 35 huku Ac Millan wakiwa nafasi ya 7 na alama
19.
0 comments:
Post a Comment