Mshambuliaji
Mfaransa anayechezea Atletico Madrid Antoine Griezmann anataka kujua
hatima yake katika klabu hiyo kabla ya kusafiri kwenda kucheza Kombe la
Ufaransa. Mchezaji huyo wa miaka 27 amehusishwa na kuhamia Barcelona.
(L'Equipe kupitia Sky Sports)
Tottenham nao wanakusudia kutumia
kifungu cha £3m kumfungua Jonny Evans kutoka kwa mkataba wake West Brom
iwapo timu hiyo itashushwa daraja. Mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka
Ireland Kaskazini huenda pia akatafutwa na Arsenal. (Telegraph)
Juventus
wamesitisha juhudi zao za kumtafuta beki kamili wa Uhispania
anayechezea Arsenal Hector Bellerin, 23. Hii ni kwa sababu wana imani
kwamba watafanikiwa kumchukua beki Mwitaliano Matteo Darmian, 28, kutoka
kwa Manchester United. (Goal) Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Hector Bellerin
Mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez, 29, anataka
kurejea katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya kutofanya vyema
akiwa kwa mkopo Deportivo La Coruna. Mhispania huyo alizomewa na
mashabiki majuzi baada yake kuendelea kutofanya vyema. (Independent)
Kipa
wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak amesema hana uhakika iwapo
atasalia katika klabu hiyo msimu ujao. Arsenal wanataka sana mlindalango
huyo wa miaka 25 ajiunge nao kuchukua nafasi ya Petr Cech, 35,
atakapostaafu. (London Evening Standard) Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Jan Oblak alitia saini mkataba wa miaka sita Atletico Madrid mwaka 2014
Kipa wa Chelsea kutoka Argentina Willy Caballero,
36, atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 2019. Hata hivyo, kipa wao
nambari wani Thibaut Courtois, 25, bado anaweza kuihama klabu hiyo.
Courtois mkataba wake utafikia kikomo mwisho wa msimu. (Goal)
Kiungo
wa kati wa zamani wa Italia Andrea Pirlo huenda akapewa kazi yake ya
kwanza kabisa ya ukufunzi katika timu ya taifa iwapo mmoja kati ya Carlo
Ancelotti na Antonio Conte ndiye atapewa kazi ya kuwa meneja wa timu ya
taifa. (Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)
Paris St-Germain wanataka kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ajiunge nao kumrithi Unai Emery mwisho wa msimu. (ESPN) Bingwa wa Olimpiki mara nane Usain Bolt atafanya
mazoezi na klabu ya Borussia Dortmund inayocheza Bundesliga katika kikao
cha mazoezi ambacho kitakuwa wazi kwa umma. (Yahoo Sports)
Kiungo wa kati wa Bournemouth Lewis Cook, 21, atajishindia
£17,000 kutoka kwa babu yake iwapo atateuliwa kuchezea England dhidi ya
Uholanzi au Italia. (Yorkshire Evening Post) Na beki wa Stoke mwenye miaka 29 Erik Pieters kutoka
Uholanzi ameomba radhi baada yake kuvunja amri ya kutotoka nje kwenda
kwa burudani katika kilabu kimoja kabla ya mechi ya Stoke na Everton
wikendi iliyopita. (Stoke Sentinel)
0 comments:
Post a Comment