
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye hapo jana siku ya Jumatatu
ya Aprili 16 amekiambia chombo cha habari cha Xinhua kuwa walifikia
maamuzi ya mwisho siku ya Jumapili baada ya kugundua Zanzibar ilikiuka
sheria za mashindano kwa kusajili wachezaji wasiostahiki.
“Zanzibar imewakilisha wachezaji waliyozidi umri kwenye mchezo wa
ufunguzi wa kundi B dhidi ya Sudan siku ya Jumapili. Mchezo ambao
haukuchezwa na ndipo tukagundua wachezaji wake 12 wamezaliwa kabla ya
Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17,”
amesema Musonye.
Timu ya Zanzibar imerudishwa nyumbani na kutakiwa kulipa faini ya
Dola za Kimarekani 15,000 na kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa
la kupeleka wachezaji waliozidi umri.
Musonye ameongeza kuwa ” Fedha hizo zitapelekwa kwenye Chama cha
Mpira wa guu Kimataifa (IFA) ambao wao ndiyo wafadhili wa michuano hiyo
ya CECAFA na kuitaka Zanzibar kutoshiriki michuano yote inayosimamiwa na
Shirikisho hilo la Afrika Mashariki na Kati mpaka pale watakapo maliza
kulipa faini.”
Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Somalia siku ya Jumapili timu ya Ethiopia imepigwa faini ya Dola 5,000 na CECAFA kwa kosa kama hilo huku wachezaji wake watatu wakitakiwa kurudishwa nchini kwao.
Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Somalia siku ya Jumapili timu ya Ethiopia imepigwa faini ya Dola 5,000 na CECAFA kwa kosa kama hilo huku wachezaji wake watatu wakitakiwa kurudishwa nchini kwao.
Kwaupande wandugu zao timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Tanzania Bara, (Serengeti Boys) ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya
Uganda kwenye mechi yake kwanza ya michuano hiyo siku ya Jumapili huku
wenyeji Burundi ikipoteza kwa mabao 4 – 0 mbele ya Kenya mchezo
uliyopigwa Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment